India ishughulikie chanzo cha ukatili dhidi ya wanawake: Mtaalamu UM

Kusikiliza /

Rashida Manjoo

Huko India baada ya ziara ya siku Tisa, mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa ametaka kuchukua hatua zaidi kukabiliana na vitendo vya  ukatili dhidi ya wanawake kama anavyo ripoti George Njogopa.

 (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa Rashida Manjoo amesema wakati kuna sura inayopaswa kupongezwa kuhusiana mageuzi ya mabaraza ya kutunga sheria lakini hata hivyo mageuzi hayo yajachukua sura iliyopendekezwa na jopo la wataalamu ambalo lilitaka kupitiwa kwa sheria inayoangazia makosa ya kingono.

Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa ambaye alitembelea India katika kipindi cha April 22 hadi May1, ameitaka mamlaka za dola kuleta ufumbuzi kuhusiana na sheria na kanuni ambazo zinabeba sura ya kibaguzi na ukandamizaji dhidi ya wanawake.

Vitendo vya unyanysaji dhidi ya wanawake na wasichana vinaarifiwa kujitokeza katika mazingira mbalimbali, ikiwemo unyanyasaji unaojitokeza majumbani ambao unajumuisha madai ya kutolewa mahali, ndoa za kulazimishwa na tabia za kuwasaka wachawi.

Hata hivyo mtaalamu huyo ametambua hatua zilizoanza kuchukuliwa na serikali kushughulikia mienendo hiyo lakini akahimiza kuongeza kasi zaidi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031