Idadi ya wahamiaji waliokwama Djibouti yaongezeka: IOM

Kusikiliza /

Wahamiaji wa Kiethiopia

Kituo cha Shirika la Kimataifa la Uhamiaji cha Obock nchini Djibouti kimebanwa na mahitaji ya msaada kutokana na ongezeko la wahamiaji wa Ethiopia waliokwama nchini humo, na ambao wanaomba msaada wa kurejeshwa nyumbani.

Katika miezi ya kwanza minne mwaka huu, yapata wahamiaji 7,137 wameandikishwa kwenye kituo hicho cha kuwasaidia wahamiaji cha Obock, idadi ambayo inaonyesha ongezeko la asilimia 79, ikilinganishwa na kipindi kicho hicho mwaka 2012.

Mnamo mwaka 2012, IOM iliwarejesha kwa hiari wahamiaji 59 wa Ethiopia ambao walikuwa hatarini. Kati ya Januari na Aprili mwaka huu, imewasaidia wahamiaji 246 kurudi nyumbani. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM na anafafanua zaidi

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930