Huu ni wakati muhimu sana kwa DRC na eneo la Maziwa Makuu

Kusikiliza /

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

“Lakini makubaliano hayo ni lazima yatafsiriwe kwa vitendo. Muafaka wa amani ni lazima uzae matunda ya amani kwa watu, Dr. Kim na mimi tunasafiri katika eneo hili katika ziara ya kwanza ya aina yake kuonyesha mshikamano na uungaji wetu mkono.Kila mahali tunakokwenda tutawataka viongozi kutimiza wajibu wao”.

Ban amesema Rais Kabila anajitahidi kutimiza wajibu wake na amempongeza kwa kuanzisha mkakati wa kitaifa ambao utasaidia utekelezaji wa makubaliano hayo ikiwemo kufanya mabadiliko muhimu, kuwa na majadiliano ya kisiasa na maridhiano. Ban amemuhakikishia Rais Kabila kwamba jumuiya ya kimataifa itakuwa pamoja nao kwani watu wengi saana wameteseka kwa muda mrefu katika taifa hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031