Haki za binadamu za wahamiaji lazima zizingatiwe:EU

Kusikiliza /

Francois Crepeau

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wahamiaji, François Crépeau, leo ameonya kwamba ongezeko la kukaza uzi kuhusu suala la wahamiaji katika nchi za Muungano wa Ulaya sio mara zote linakwenda sambamba na uzingatiaji wa haki za binadamu hasa kwa wahamiaji wa kiholela.

Bwana. Crépeau amesema ndani ya taasisi na sera za mifumo ya Muungano wa Ulaya uhamiaji na udhibiti wa miapaka vimekuwa vikihusishwa na masuala ya usalama ambayo yanasisitiza ulinzi wa polisi, kujihami na uhalifu, badala ya mtazamo unaozingatia haki.

Ameyasema hayo kwenye ripoti maalumu aliyoiwasilisha kwenye baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva kuhusu udhibiti wa mipaka kwenye muungano wa Ulaya.

Tangu Mai 2012 mwakilishi huo amefanya utafiti wa mwaka mmoja kuchunguza haki za wahamiaji kwenye Ukanda wa Ulkaya na Mediteranian akijikita zaidi kwenye udhibiti wa miapaka ya nje ya Muungano wa Ulaya.

Mbali ya Brussels Bwana Crépeau alikusanya pia taarifa kwenye nchi mbili muhimu kwa suala la wahamiaji , Uturuki na Tunisia, na maeneo mawili ambayo wahamiaji huingilia Ulaya, Ugiriki na Italia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031