Gesi ya cabon angani imeongezeka sana:UNFCCC

Kusikiliza /

Katibu  mkuu kwenye makubalino ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa Christiana Figueres amelalamikia suala kuwa kuongezeka viwango vya gesi ya carbon angani vimepita kiwango cha juu zaidi ambapo ametaka hatua kuchukuwa kukabiliana na madabiliko ya hali ya hewa yanayoendelea kushuhudiwa.

Amesema kuwa viwango vya sasa vya gesi ya Carbon vya mianne kwa milioni ni vya kihistoria  na sasa ulimwengu umeingia wakati wa hatari. Amesema kuwa ulimwengu ni lazima ugutuke na kuchukua hatua kwa usalama wa mwanadamu  na mandeleo ya kiuchumi.

Amesema kuwa kinachohitajika ni kuwekwa sera ambazo zitakabiliana na hali iliyo sasa. Ameongeza kusema kuwa bado kuna fursa ya kuondoa athari za mabadiliko ya hali ya hewa kupitia kwa pande tatu kuu  zikiwemo jamii ya  kimataifa, serikali na sekta za biashara na fedha.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031