Baraza la Usalama lajadili hali nchini Bosnia na Herzegovina

Kusikiliza /

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo limekutana leo kujadili hali ya sintofahamu inayoendelea kushamiri katika siasa za nchi ya Bosnia na Herzegovina. Joshua Mmali ana maelezo zaidi.

(RIPOTI YA JOSHUA MMALI)

Nchi yaBosnianaHerzegovinaimepiga hatua za maendeleo kufuatia baa la vita liloighubika katika miaka ya tisini, amesema Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuihusu nchi hiyo, Valentin Inzko, wakati akilihutubia Baraza la Usalama ambalo limekutana kuangazia hali ya sintofahamu inayoikumba hali ya baadaye ya kisiasa nchini humo

Licha ya maendeleo hayo, Bwana Inzko amesema bado kuna kazi nyingi ya kufanya, na uwepo wa Umoja wa Mataifa bado ni muhimu, ili kuhakikisha kuwa msingi uliowekwa wa maendeleo unalindwa na kutumiwa kufikia ufanisi zaidi.

(SAUTI YA INZKO)

 ”Ukanda mzima unaendelea, lakini Bosnia na Herzegovina imekwama. Mwaka baada ya mwaka, viongozi wake wa kisiasa wameikwamisha nchi hiyo kwa kushindwa kufikia makubaliano muhimu, yanayohitajika kuiendeleza nchi na kukabiliana na matatizo sugu ya kiuchumi na kijamii yanayoikumba nchi hiyo. Nchi hiyo inahitaji uwepo wa jamii ya kimataifa, subira na mtazamo wa muda mrefu.”

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031