Baraza la usalama la laani vikali mashambulizi dhidi ya MONUSCO

Kusikiliza /

Baraza la Usalama

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali mashambulizi ya kuwalenga na kujaribu kuwateka wafanyakazi wa mpango wa Umoja wa mataigfa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO yanayofanywa na watu wasiojulikana.

Mashambulizi hayo yalikuwa ni dhidi ya msafara wa wanjeshi ukitoka Walungu kuelekea Bukavu Kivu ya Kusini mapema jana na kusababisha kifo cha mlinda amani mmoja kutoka Pakistan.

Kufuatia shambulio hilo wajumbe wa baraza wametuma salamu za rambirambi kwa familia za mlinda amani huyo, serikali ya Pakistan na kwa MONUSCO na wameitaka serikali ya Congo kufanya uchunguzi wa tukio hilo na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wahusika.

Wajumbe hao pia wamerejea uamuzi wao wa kuendeleza vikwazo vilivyoainishwa kwenye azimio namba 2078 kwa watu binafsi na makundi ambayo yanapanga, kufadhili au kushiriki katika mashambulio dhidi ya walinda amani wa MONUSCO  na kuahidi kuendelea kuisaidia MONUSCO na kuzitolea wito pande zote nchini DRC kutoa ushirikiano unaohitajjika kwa mpango huo wa Umoja wa Mataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031