Baraza la usalama la laani utekaji wa wafanyakazi wa UNTSO Golan

Kusikiliza /

Wanajeshi, UNTSO

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali tukio la Mai 15 ambapo kundi la watu wenye silaha wanaoipinga serikali liliwateka wanajeshi watatu wa Umoja wa Mataifa wa mpango wa upatanishi na uangalizi huko Golan.Watu hao wenye silaha waliwashikilia wanajeshi wa UNTSO kwa saa kadhaa na kupora katika ofisi za mpango huo.

Wajumbe wa baraza wamesema wanalichukulia tukio hilo kama la kutia hofu ukizingatia kwamba hilo lilikuwa ni tukio la tatu katika kipindi cha miezi miwili.

Wajumbe wa baraza la usalama wamezitaka pande zote kushirikiana na mpango wa UNDOF na ule wa uangalizi wa UNTSO Golan kwa amani na kuuwezesha kutekeleza mmajukumu yake kwa uhuru na kuhakikishiwa usalama wa wafanyakazi wake.

Pia baraza limerejelea kuhakikikishia mpango wa UNDOF na UNTSO ushirikiano na msaada usio na mashariti ili kuhakikisha malengo yao yanatimia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2015
T N T K J M P
« jul    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31