Baraza la haki za binadamu kujadili Syria

Baraza la haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu mjini Geneva Jumatano wiki hii litafanya mjadala wa dharura kuhusu hali ya haki za binadamu nchiniSyrialicha ya kupingwa vikali mjadala huo na serikali za Syria,Cuba naVenezuela.

 

Ombi la kufanyika mkiutano utakaojadili sualahilolimewasilishwa kwa pamoja na serikali za

Turkey,Qatar na Marekani Ijumaa iliyopita. Baraza limeombwa kujadili ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea nchiniSyriana hususani mauaji ya hivi karibuni Al Qusayr.

 

Mwakilishi wa Qatari Bi Alya Ahmed Saif Al-Thani amesema mjadala huo ni muhimu na ni jambo la dharura kwa sababu hali inazidi kuwa mbaya huku waathirika wakumbwa walkiwa ni wanawake na watoto.

 

Akipinga kufanyika kwa mjadala huo mwakilishi waSyriaamesema nchi ambazo zimeomba kufanyika mkutano huo zinaipinga serikali yaSyriakwa kutoa mafunzo na msaada kwa waasi na magaidi wanaopigana nchiniSyria.

 

 

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29