Baraza Kuu lajadili maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza /

 Hapa mjiniNew York, Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekutana kujadili maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabianchi, likiangazia masuala ya maji na nishati. Joshua Mmali ana maelezo zaidi

(RIPOTI YA JOSHUA MMALI)

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Vuk Jeremic, amesema haiwezekani tena wanadamu kuendelea tu na shughuli za kawaida bila kujali mazingira, kwani ukuaji unaoandama mkondo wa sasa hautoleta utajiri, bali utawaelekeza kwenye baa kubwa. Bwana Jeremich amesema hayo leo kwenye mkutano wa Baraza Kuu kuhusu maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabianchi. Ameongeza kuwa kinachohitajika ni kuandama njia mpya ya kufikia maendeleo endelevu, kwa kubuni ushirikiano mpya wa kimataifa ambao hauiachi nyuma nchi yoyote, wala kuliruhusu taifa lolote kujiondoa kwenye njia hiyo. Rais huyo wa Baraza kuu amesema hali hii inahitaji mwelekeo mpya, na mikakati mipya.

 SAUTI YA VUK JEREMIC

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930