Baraza kuu la Umoja wa Mataifa laiweka Polynesia kuwa eneo lilo kwenye orodha ya Umoja wa Mataifa ya kuwa huru

Kusikiliza /

Kikao cha Baraza Kuu

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita lilipiga kura ya kuamua kuviondoa visiwa vya Polynesia kutoka kwa ukoloni wa Ufaransa na kuiomba serikali ya Ufaransa kufanya hima .

Kupitia kwa azimio lililopendekezwa na visiwa vya Nauru,Tuvaluna Solomon baraza kuu liliamua kuwa watu wa Polynesia wana haki ya kuwa huru kuambatana na mkataba wa Umoja wa Mataifa. Mwezi Juni mwaka 2011 baraza la mawaziri kwenye eneo la Polynesia  lilipitasha azimio la kuwa huru kupitia kwa mpango kwa Umoja wa Mataifa.  

Pia kupitia kwa azimio lililopitishwa na nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa linaiomba kamati  maalum ya Umoja  huo ya kumaliza ukoloni kungazia eneo la Polynesia na kuripoti kwa baraza kuu kwenye kikao chake cha 68. Azimio hilo pia linaiomba serikali ya Ufaransa kuendeleza mazungumzo na eneo la Polynesia ili kuharakisha mikakati ya kulifanya eneo hilo huru ambapo wakati na mipangilio yote ya kuwa huru itafanyika.

Hata hivyo mataifa ya uingereza, Marekani , Ujerumani na Uholanzi yalijiondoa kutoka kwa kura hiyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930