Ban ataka wafanyakazi wa UNDOF waachiliwe

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani vikali kushikiliwa kwa walinda amani wanne wa ujumbe wa UNDOF nchini Syria na watu wenye silaha kwenye eneo la Al Jamla ambalo ni gumu kufikika, na kutaka waachiliwe huru mara moja.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nersirky amesema Bwana Ban amewakumbusha wahusika wote katika mzozo wa Syria kuwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa, UNDOF umepewa majukumu ya uangalizi wa mkataba wa kuweka chini silaha kati ya Israel na Syria.

(SAUTI YA MARTIN)

Tunaweza kuthibitisha kwamba walinzi wanne wa amani kutoka katika kikosi cha umoja wa mataifa cha walinda amani kwenye maeneo huru ya uangalizi waliwekwa kizuizini leo na kikosi chenye silaha ambacho bado hakijafahamika wakati wakiwa kwenye doria katika eneo liliotengwa karibu na eneo no 86 Aljamla, askari hao wane kini kutoka jeshi la Uphipino na juhudi zinaendelea ili kuwakwamua.”

Bwana Ban pia ametoa wito kwa wote kuheshimu uhuru wa wafanyakazi wa UNDOF, pamoja na usalama wao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031