Ban ampongeza mfalme mpya wa uholanzi

Kusikiliza /

Katibu Mkuu, UM na mfalme wa Uholanzi(picha ya maktaba)

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amempongeza Willem-Alexander wakati wa kuapishwa kwake kama mfalme wa Uholanzi taifa lililo mshirika mkubwa wa Umoja wa Mataifa . Kupitia taarifa yake  Ban aliwatakia heri mfale  Willem-Alexander na malikia Maxima na mafanikio wakati wanapoanza kutekeleza majukumuyao. Kwa upande mwingine Ban amesema kewa lengolakekuuni kuunga mkono jitihada zinazoendelea za kutimizwa kwa malengo ya maendeleo ya milenia. Umoja wa Mataifa unaitaka jamii ya kimataifa kuweka mikakati ya kutimiza malengo manane ya kumaliza umaskini yanayojulikanakamamalengo ya maendeleo ya milenia huku zikiwa zimesalia chini ya siku 1000 kabla ya mwaka 2015. Ban pia pia amezungumzia umuhimu wa mji wa Hague ulio makao kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC  na mahakama zingine za kimataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031