Nyumbani » 21/05/2013 Entries posted on “Mei 21st, 2013”

Zaidi ya watu milioni 7 sasa wanapata matibabu dhidi ya HIV Afrika: UNAIDS

Kusikiliza / Vita dhidi ya Ukimwi

  Wakati Muungano wa nchi za Afrika (AU) unapoanza mkutano wake wa 21 na kuadhimisha miaka 50 ya kuungana kwa bara Afrika, Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu virusi vya HIV na UKIMWI (UNAIDS), umetoa ripoti mpya inayoonyesha hatua zilizopigwa katika kupiga vita UKIMWI barani humo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya [...]

21/05/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu asikitishwa na janga la huko Oklahoma

Kusikiliza / madhara ya tufani huko Oklahoma

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewandikia barua Gavana wa jimbo laOklahomanchini Marekani kufuatia janga la vifo na majeruhi lililotokana na tufani iliyopiga eneohilosiku ya Jumatatu. Bwana Ban amesema yeye binafsi na Umoja wa Mataifa kwa ujumla wako pamoja na wakazi wa jimbo hilo na kwamba wako tayari kutoa msaada wowote kadri [...]

21/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wajielekeza kurejesha amani Mali.

Kusikiliza / MALI2

Mali taifa lililoko magharibi mwa Afrika limekumbwa na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe iliyosababisha kuporomoka kwa uchumi wa nchi hiyo. Ungana na Joseph Msami katika ripoti inayoangazia juhudi za Umoja wa mataifa katika kurejesha amani nchini humo.

21/05/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Bi Robinson ahofia kuzuka tena mapigano mashariki mwa DRC

Kusikiliza / Mary Robinson

  Mwakilishi wa Katibu Mkuu katika nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, Mary Robinson, ameelezea wasiwasi wake kufuatia kuzuka tena kwa mapigano hivi karibuni katika maeneo karibu na mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC, akitolea wito uungwaji mkono wa juhudi zote zinazoendelea ili kuleta amani na utulivu katika ukanda huo. [...]

21/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sekta thabiti ya kilimo itasaidia kuimarisha afya: AU

Kusikiliza / Nkosazana Dlamini-Zuma

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma amehutubia baraza la afya la shirika la afya duniani, WHO hukoGeneva, Uswisi na kusema kuwa Umoja wa Afrika unaamini kuwa kuboresha sekta ya kilimo ni njia mojawapo ya kuimarisha sekta ya afya. Dkt. Nkosazana amesema sekta hakika ya kilimo itawezesha kupatikana fedha za ziada kwa ajili [...]

21/05/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban ahitimisha ziara Msumbiji

Kusikiliza / Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Armando Emilio Guebuza akutana na KM wa UM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amehitimisha ziara yake nchini Msumbiji, huku akiisifu nchi hiyo kwa hatua ilizopiga kimaendeleo. Mengi zaidi na Joshua Mmali TAARIFA YA JOSHUA MMALI Akihitimisha ziara yake nchini Msumbiji, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema katika kipindi cha miongo miwili ilopita, nchi hiyo imepiga hatua, na kuonyesha kuwa nchi inaweza [...]

21/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yahaha kudhibiti mlipuko wa kipindupindu Niger.

Kusikiliza / Biashara ya maji Niger

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linahaha kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwenye kwambi za wakimbizi nchiniNiger, tangu serikali ya nchi itangaze mlipuko wa ugonjwa huo tarehe 11 mwezi huu. Mlipuko wa kipindupindu magharibi mwaNigerhadi sasa umesababisha vifo vya watu Saba wamekufa wakiwemo wakimbizi wawili kutokaMaliwaliokuwa wakiishi kambi ya Mangaize. Melissa [...]

21/05/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF kuanza kutoa chanjo ya dharura kukabili surua CAR

Kusikiliza / Mtoto apokea chanjo

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF pamoja na washirika wake linajiandaa kuanzisha kampeni ya dharura kwa ajili ya njanjo kukabili tishio la ugonjwa wa surua ambao ameripotiwa kuwakumba watoto kadhaa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.Vipimo vilivyofanywa mwezi April mwaka huu katika mji mkuu Bangui vimebaini watoto 8 wamekumbwa na ugonjwa huo. [...]

21/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma ya afya kwa wote ni msingi wa kutokomeza umaskini: Benki ya Dunia

Kusikiliza / Jim Yong Kim

Benki ya dunia imetaka jitihada za kimataifa zichukuliwa katika kuhakikisha kila mtu duniani ana uwezo wa kupata huduma bora za afya. Akihutubia kikao cha mwaka cha baraza kuu la shirika la afya duniani, WHO huko Geneva, Uswisi, Rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim amesema ili kufikia lengo la kutokomeza ufukara mwaka 2030, nchi [...]

21/05/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Changamoto za kiuchumi zazorotesha usalama wa chakula na hali ya lishe Misri: WFP

Kusikiliza / SOko la vyakula, Misri

Ripoti mpya iliyotolewa Jumanne inaonyesha kuzidi kuongezeka kwa umaskini na ukosefu wa uhakika wa chakula nchini Misri kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Grace Kaneiya ana ripoti zaidi. (SAUTI YA GRACE) Ripoti hiyo iliyoandaliwa kwa ushirika kati ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP, taasisi ya kimatifa ya utafiti wa sera za chakula na [...]

21/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM na harakati za kudhibiti ukatili wa kingono mashariki kwa DRC

Kusikiliza / IOM

Wakati Umoja wa Mataifa ukiripoti kuendelea kushamiri kwa vitendo vya ukatili wa kingono huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limeendeleza harakati zake za kuhamasisha jamii ya eneo hilo kama njia moja ya kukabiliana na ukatili huo wa kingono.IOM ambayo imeanza harakati hizo tangu mwaka 2010 baada [...]

21/05/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wasyria milioni 8.3 wanahitaji msaada kuishi

Kusikiliza / Familia za wasyria wanokimbia mipakani/UNHCR

Karibu wasyria nusu milioni kwa sasa wanategemea misaada ya kibinadamu kuishi kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Alice Kariuki na taarifa kamili   (TAARIFA YA ALICE)   UNHCR inasema kuwa zaidi ya wasyria milioni 8.3 wanapokea misaada ya kibinadamu kama wakimbizi kwenye nchi majirani au kama wakimbizi wa ndani. [...]

21/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031