Nyumbani » 17/05/2013 Entries posted on “Mei 17th, 2013”

Ban ateua wawakilishi wake maalum huko Mali na Cote D'Ivoire

Kusikiliza / Mkuu mpya wa UNOCI, Bi.Aichatou Mindaoudou

Ujumbe wa umoja wa mataifa wa kuweka utulivu huko Mali, MINUSMA ulioanzishwa mwaka huu umepata kiongozi ambaye pia atakuwa mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon, naye si mwingine bali ni Bert Koenders kutoka Uholanzi. Bwana Koenders anaenda kushika wadhifa huo akitokea hukoCote D'Ivoirealikokuwa akimwakilisha katibu Mkuu kwenye ofisi ya Umoja huo, UNOCI tangu Oktoba [...]

17/05/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Hatua madhubuti zichukuliwe ili kuhakiksha maisha yaliyo bora mijini:UNEP

Kusikiliza / dandora2

Wakati idadi ya watu inapoendelea kuongezeka duniani, nayo idadi ya watu mijini inazidi kuongezeka. Watu zaidi wanaendelea kuhamia mijini kutafuta ajira, wakati katika takriban nchi zote zinazoendelea, miundo msingi, ikiwemo ya usafiri, nishati na makao haikupangwa ikilinganishwa na ilivyo kwenye nchi zilizostawi. Kwa mujibu wa Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, hatua madhubuti [...]

17/05/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Haile Menkerios atakuwa Mkuu wa Ofisi ya UM kwenye AU: Ban

Kusikiliza / Haile  Menkerios

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemteua Bwana Haile Menkerios wa Afrika Kusini kuwa mwakilishi wake maalum kwa Muungano wa nchi za Afrika, AU, na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa kwenye AU. Bwana Menkerios pia ataendelea kushikilia wadhafa wake kama Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini Sudan na Sudan Kusini. Menkerios [...]

17/05/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yapata Kamanda mpya, ni Carlos Alberto Dos Santos Cruz

Kusikiliza / Lt. jenerali Carlos Alberto Dos Santos Cruz

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemteua Luteni Jenerali Carlos Alberto Dos Santos Cruz wa Brazil kuwa Kamanda Mkuu wa ujumbe wa Umoja huo unaoweka utulivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, MONUSCO.Anaziba nafasi iliyoachwa na Luteni Jenerali Chander Prakash Wadhwa wa India, aliyemaliza kipindi cha uhudumu tarehe 31 mwezi Machi mwaka [...]

17/05/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban na Putin wajadili Syria, Afghanistan na Mashariki ya Kati

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Rais Vladmir Putin wa Urusi

Naunga mkono makubaliano kati ya Urusi na Marekani ya kuandaa kongamano la kimataifa kuhusu Syria, na hiyo ni moja ya kauli za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alizotoa wakati wa mazungumzo yake na Rais Vladmir Putin wa Urusi huko Sochi hii leo. Bwana Ban amesema kongamano hilo litasaidia pande husika huko Syria kuanza [...]

17/05/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Rais wa Nigeria atangaza hali ya hatari katika majimbo ya Mashariki

Kusikiliza / Mwanamumue asimama mahala nyumba yake ilipoharibiwa kufuatia machafuko, Nigeria

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ametangaza hali ya hatari katika majimbo matatu yaliyoko Mashariki mwa nchi hiyo kufuatia uasi unaendeshwa na kundi la Boko Haramu ambao wanahatirisha mustakabala wa taifa. Tayari kamishna ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imelaani vikali matukio ya mashambulizi yanayoendeshwa na kundi hilo ambalo linatajwa kuwa na mafungaano pia [...]

17/05/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ajadili suala la Syria na viongozi wa Urusi huko Sochi

Kusikiliza / Ban Ki-moon na Sergei Lavrov

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov wameafikiana kwamba mkutano wa kimataifa kuhusu Syria ufanyike haraka iwezekanavyo ili kuzisaidia pande husika katika machafuko kufanya majadiliano. Joshua Mmali na taarifa kamili Suluhu litokanalo na mazungumzo ya kisiasa ndiyo njia pekee itakayoumaliza mzozo wa Syria, amesema [...]

17/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

TEKNOHAMA ichochee usalama barabarani: Ban

Kusikiliza / Ajali za barabarani zinasababisha vifo vya zaidi ya watu milioni moja

Katika kilele cha siku ya jamii habari duniani hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe unaotaka maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, TEKNOHAMA yawe kichocheo cha kuimarisha usalama barabarani.Bwana Ban amesema msimamo huo unazingatia takwimu za hivi punde ya kwamba watu ajali za barabarani kila mwaka husababisha vifo vya [...]

17/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ILO yachochea usawa maofisini kwa waliobadili jinsi na wapenzi wa jinsia moja

Kusikiliza / ILO, kuongeza kasi, usawa maofisini

Shirika la kazi duniani, ILO limesema linaongeza kasi ya kutokomeza vitendo vya watu kubaguliwa kazini kwa misingi ya mwelekeo wao wa jinsia au mapenzi.Mkurugezi Mkuu wa ILO Guy Rider amesema hatua za kuhakikisha usawa kwa wanawake na walemavu sehemu za kazi zimeonyesha matumaini na maendeleo yaliyopatikana kuhakikisha mashoga na waliobadili jinsia wanapata haki sawa kwenye [...]

17/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tokomeza ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja: Pillay

Kusikiliza / homophobia2

Katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsi zao, Umoja wa Mataifa umetaka nchi wanachama kuchukua hatua zaidi kutokomeza vitendo vya kikatili na ghasia dhidi ya makundi hayo. Ripoti ya Jason Nyakundi inafafanua zaidi. (TAARIFA YA JASON) Kamishina mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja [...]

17/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yajiandaa kuwapelekea misaada wakimbizi nchini Chad

Kusikiliza / sudan refugees2

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linandaa misaada kwa maelfu ya wakimbizi kutoka jimbo la Darfur walioingia mashariki mwa Chad wakati hofu ikitanda kuwa mvua zinazonyesha huenda zikazuia kufikiwa kwa eneo hilo. Hivi majuzi karibu watu 30,000 walikimbia ghasia za kikabila kaskazini na magharibi mwa Darfur nchini Sudan. Taarifa ya Alice Kariuki [...]

17/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yaongeza msaada wa chakula kaskazini mwa mali

Kusikiliza / WFP, yaongeza msaada wa chakula, Mali

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linaongeza operesheni zake za msaada wa dharura Kaskazini mwa Mali na hususani maeneo ya Timbuktu, Gao na Kidal.Katika maeneo hayo moja kati ya kila familia tano inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula. WFP inasema kufikisha misaada ya kibinadamu katika maeneo hayo bado ni changamoto na inatathiminiwa kila siku [...]

17/05/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama la laani utekaji wa wafanyakazi wa UNTSO Golan

Kusikiliza / Wanajeshi, UNTSO

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali tukio la Mai 15 ambapo kundi la watu wenye silaha wanaoipinga serikali liliwateka wanajeshi watatu wa Umoja wa Mataifa wa mpango wa upatanishi na uangalizi huko Golan.Watu hao wenye silaha waliwashikilia wanajeshi wa UNTSO kwa saa kadhaa na kupora katika ofisi za mpango huo. Wajumbe wa baraza wamesema [...]

17/05/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM waahidi kuipiga jeki Tanzania kuboresha lishe bora

Kusikiliza / Baadhi ya vyakula

Umoja wa Mataifa umeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Tanzania kukabiliana na tatizo la lishe bora hasa wakati huu ambapo dunia inapiga mwendo kuelekea kwenye malengo ya maendeleo ya mellenia. George Njogopa na taarifa zaidi.(TAARIFA YA GEORGE) Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya kitaifa yenye lengo la kuboresha hali ya lishe Mwakilishi wa [...]

17/05/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dozi moja tu yatosha kukinga homa ya manjano: WHO

Kusikiliza / homa ya manjano

Shirika la afya duniani WHO linasema sasa dozi moja tuu ya chanjo ya homa ya manjano inatosheleza kumpa mtu kinga ya maisha dhidi ya maradhi hayo. Masharti ya sasa ya kimataifa yanahitaji mtu anayesafiri au kuishi katika nchi ambazo zinaathirika na homa ya manjano kupata chanjo mbili ya kwanza na ya marudio miaka kumi baadaye. [...]

17/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930