Nyumbani » 14/05/2013 Entries posted on “Mei 14th, 2013”

Kukata na kula moyo wa maiti Syria ni uhalifu ulokithiri: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

      Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay, amesema video kutoka Syria inayoonyesha kiongozi wa waasi akikata na kuula moyo wa mwanajeshi wa serikali inabainisha kitendo cha uovu wa kupindukia. Bi Pillay amesema kukatakata maiti wakati wa vita ni uhalifu wa kivita, na kuongeza kuwa ingawa bado ni vigumu kuthibitisha video hiyo, [...]

14/05/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Athari za teknohama zaangaziwa Geneva

Kusikiliza / watoto na intaneti

Wakati dunia itaadhimisha siku ya kimataifa ya Jamii habari tarehe 17 mwezi huu, wawakilishi wa nchi wanachama wa Taasisi ya kimataifa ya mawasiliano ITU, taasisi za kimataifa, na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa wanamkutana mjini Geneva, Uswisi, katika mkutano wa siku tatu unaolenga kuchukua mrejesho wa  lengo lililowekwa na wanachama hao la kuhakikisha dunia inafaidika [...]

14/05/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Usalama huko Pibor, Kusini Sudan wazidi kuzorota: UNMISS

Kusikiliza / Wakazi wa eneo la Pibor

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake juu ya kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama kwenye mji wa Pibor na viunga vyake huko huko jimbo la Jonglei Sudan Kusini. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS umetaja vitendo kama vile uporaji kama wa vyakula, ghasia na watu kukimbia makazi yao kuwa ni mambo yanayozoresha usalama [...]

14/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali Eritrea ifuatiliwe kwa karibu: Mtaalam wa UM

Kusikiliza / Sheila B. Keetharuth

Mtaalam maalum mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Eritrea, Sheila B. Keetharuth, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kufuatilia kwa karibu sana hali nchini Eritrea hadi hapo mabadiliko kamili yatakapodhihirika nchini humo. Mtaalam huyo ambaye amekamilisha ziara ya siku kumi nchini Ethiopia na Djibouti, ilokusudiwa kukusanya maelezo kutoka kwa [...]

14/05/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban afanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa CAR

Kusikiliza / Ban Ki-moon akutana na Waziri mkuu wa CAR, Tiangaye

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Nicolas Tiangaye, na kuelezea kuunga kwake mkono na kutambua uhalali wa mamlaka ya Waziri huyo mkuu, kutokana na makubaliano ya Libreville na azimio la N'Djamena. Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wake, Bwana Ban [...]

14/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yasaidia kurejea makwao wavuvi wa Kenya waliokwama Puntland

Kusikiliza / Shughuli za uvuvi nchini Somalia

Mabaharia sita raia wa Kenya waliokuwa wametelekezwa na mwajiri wao kwenye eneo la Basaso Puntland nchini Somalia mwezi Novemba mwaka 2012 watarejea nyumbani  kesho Jumatano kupitia msaada wa Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Wavuvi hao ambao walikuwa kati ya kundi lililokuwa ndani mwa chombo kimoja cha uvuvi waliondoka mjini Mombasa Kenya kwa shughuli ya uvuvi [...]

14/05/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili hali nchini Bosnia na Herzegovina

Kusikiliza / Valentin Inzko

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo limekutana leo kujadili hali ya sintofahamu inayoendelea kushamiri katika siasa za nchi ya Bosnia na Herzegovina. Joshua Mmali ana maelezo zaidi. (RIPOTI YA JOSHUA MMALI) Nchi yaBosnianaHerzegovinaimepiga hatua za maendeleo kufuatia baa la vita liloighubika katika miaka ya tisini, amesema Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja [...]

14/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR Burundi imefungua kambi mpya ya wakimbizi wa Congo:UNHCR

Kusikiliza / UNHCR Burundi kuweka kambi mpya kwa ajili ya wakimbizi

Nchini Burundi, wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambao wanakimbilia usalama wao kutoka mashariki mwa nchi hiyo, watawekwa kwenye kambi mpya ya Kavumu katika mkoa wa Cankuzo.Kambi hiyo ambayo itafunguliwa hapo kesho Jumatano, Mei 15 na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Ina uwezo wa kuhifadhi hadi wakimbizi 13,000, na inatarajiwa kuwa [...]

14/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara ya kilimo ni fursa ya ajira:ILO/UNCTAD

Kusikiliza / Kuna fursa ya ajira katika kilimo

Kitabu kipya kilichohaririwa na shirika la kazi duniani ILO na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya uchumi na biashara UNCTAD kinasisitiza kwamba biashara ya kilimo inaweza kuwa fursa nzuri ya kuunda nafasi za ajira  na kutokomeza umasikini duniani.Kitabu hicho chenye kichwa "kugawana mavuno:kilimo, biashara na ajira"kimetolewa leo. Kitabu hicho ambacho ni matokeo ya [...]

14/05/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa UM Syria:UNICEF/WFP

Kusikiliza / Msaada wa dharura wahitajika

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamepeleka wajumbe wake kwenye eneo la Al-houle nchiniSyria, ambako zaidi ya watu 100, wakiwemo watoto 49, waliuawa katika machafuko, ndani ya kipindi cha siku moja mnamo Mei mwaka 2012.Huu ndio ujumbe wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kwenda katika eneo hilo, ambalo limekuwa halifikiki kwa miezi mingi tangu mapigano yalipoanza. [...]

14/05/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Virusi vya polio isiyofahamika vyabainika Somalia, WHO yachunguza

Kusikiliza / Mtoto apokea chanjo, Somalia

Uchunguzi umeanzishwa kuhusu ripoti ya kuwepo kwa virusi vivyojulikana aina ya WPV1 vya ugonjwa wa polio katika eneo la Banadir nchini Somalia.Shirika la afya duniani WHO linasema hivi ni virusi vya aina yake kuripotiwa nchini Somalia tangu mwezi Machi mwaka 2007 . Assumpta Massoi na taarifa kamili. (RIPOTI YA ASSUMPTA MASSOI) Virusi hivyo vilitenganishwa kutoka [...]

14/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani vikali shambulizi la Benghazi

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulizi la bomu ambalo lilipigwa katika mji wa Benghazi nchini Libya ambalo lilisababisha watu kadhaa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.Baraza hilo limesema kuwa limepokea kwa masikitiko makubwa tukio la shambulizo hilo lililofanyika May 13 na limewapa pole waathirika na serikali kwa ujumla. Limetaka wahusika wa tukio [...]

14/05/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tufani Mahasen kuikumba Myanmar na Bangladesh

Kusikiliza / Mwelekeo wa tufani Mahasen

Nchini Bangalesh na Myanmar mapema leo wametangaza tahadhari na mikakati ya kukabiliana na tufani Mahasen inayotarajiwa kukumba maeneo hayo muda si mrefu. Mashirika ya Umoja wa Mataifa hususani lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR yamesema yako tayari kuzisaidia nchi hizo  ambapo linasema linatiwa hofu na hali ya wakimbizi wa ndani katika jimbo la Rakhine. Wakimbizi takribani [...]

14/05/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa DRC kutoka Angola wasaka huduma za kibinadamu: IOM

Kusikiliza / Baadhi ya wakimbizi wa DRC walioko Angola

Takribani wakimbizi Elfu  40 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, wanaorejea nyumbani kutokaAngolawametindikiwa na huduma za kibinadamu katika eneo liitwalo Kamako mpakani mwa nchi mbili hizo. Wakimbizi hao wanarejea nyumbani kufuatia ilani ya serikali yaAngolaya kuwataka wawe wamerejea makwao ifikapo kesho tarehe 15 mwezi huu.  Wakimbizi hao waliofurika katika eneo hilo wanalazimika kukimbilia mashuleni [...]

14/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria dhidi ya mashirika yasiyo ya kibiashara Urusi ni kandamizi: wataalamu huru UM

Kusikiliza / Maina Kiai, Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa

Wataalamu huru watatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za bindamu wameeleza wasiwasi wao mkubwa juu ya mazingira ya kihasama ambayo mashirika yasiyo ya kibiashara nchini Urusi yanakumbana nayo kutokana na sheria mpya iliyopitishwa mwezi Novemba mwaka jana.  Wataalamu hao kuhusu uhuru wa kujumuika, utetezi wa haki za binadamu na uhuru wa kujieleza wametaka sheria [...]

14/05/2013 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Visa vipya vya virusi vya Corona vyabainika Saudia

Kusikiliza / Madaktari wakichunguza X-ray

Wizara ya afya ya Saudi Arabia leo Jumanne imetangaza kusajiliwa kwa visa vingine vipya vinne vya virusi vya Corona  kwenye jimbo la Mashariki mwa nchi hiyovinavyosababisha matatizo ya kupumua. Wizara hiyo inasema mgonjwa mmoja aliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupatiwa matibabu na wengine watatu bado wako hospitali. Shirika la afya duniani WHO linasema limekuwa likitathimini idadi [...]

14/05/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930