Nyumbani » 07/05/2013 Entries posted on “Mei 7th, 2013”

Ubunifu wa sekta binafsi unaweza kusaidia kukabiliana na changamoto za sasa: Ban

Kusikiliza / Mama na mwanawe, Dharka/UN picha

Umoja wa mataifa utahakikisha ya kwamba unatumia vyema nafasi na ubunifu wowote ule uliopo katika kizazi cha sasa. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki-moon kwenye tukio lililomkutanisha na wakurugenzi wakuu wa mashirika makubwa ya kibinafsi kama Benki ya JPMorgan Chase, na kampuni nyingine za kimataifa kama vile Johnson $ [...]

07/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za Afrika Kaskazini zapatiwa fedha kuendeleza mradi wa nishati ya sola

Kusikiliza / Nishati ya sola

Nchi za Afrika Kaskazini zimetengewa kiasi cha dola za Marekani bilioni 7.6 toka kwa fuko  maalumu la ufadhili miradi ya hali ya hewa, ili kuendeleza mradi wa nishati ya umeme wenye ukubwa wa megawatt 1,120. Mradi huo ambao unategemea kutumia nguvu za sola, unatekelezwa katika nchi sita Algeria, Misri, Jordan,Libya, Morocco na Tunisia. Rais wa [...]

07/05/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ataka wafanyakazi wa UNDOF waachiliwe

Kusikiliza / Walinda amani, UNDOF

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani vikali kushikiliwa kwa walinda amani wanne wa ujumbe wa UNDOF nchini Syria na watu wenye silaha kwenye eneo la Al Jamla ambalo ni gumu kufikika, na kutaka waachiliwe huru mara moja. Akiongea na waandishi wa habari mjini New York msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nersirky [...]

07/05/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Visa zaidi vya maambukizi ya homa ya A(H7N9) vyaripotiwa China

Kusikiliza / Utafiti kuhusu virusi vya A(H7N9)

        Wizara ya Afya na Tume ya Uzazi wa Kupanga nchini China imelifahamisha Shirika la Afya Duniani, WHO kuwa imethibitisha visa viwili zaidi vya maambukizi ya virusi vya homa ya A(H7N9). Mgonjwa wa kwanza ni mwanamume mwenye umri wa miaka 69 kutoka mkoa wa Fujian, ambaye alianza kuumwa mnamo Aprili 29, naye [...]

07/05/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tanzania yasema haitishiki na vitisho vya M23

Kusikiliza / Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernard Membe

Mwishoni mwa wiki, serikali ya Tanzania ilipata ridhaa ya Bunge la nchi hiyo ya kupeleka vikosi vyake kuungana na brigedi iliyoundwa kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuweka utulivu huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo, DRC. Brigedi hiyo itajumuisha pia vikosi kutoka Afrika Kusini na Malawi [...]

07/05/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Maelfu wakabiliwa na ukame visiwani Marshall

Kusikiliza / geography-of-marshall-island0

Takribani watu elfu 50 wanakabiliwa na ukame katika visiwa vya Marshal vilivyoko karibu na bahari ya Pasific kutokana na ukosefu wa mvua jambo linalosababisha baadhi ya familia kutumia litre 3 nukta nane za maji kwa siku ambacho ni nusu ya kiwango cha kimataifa cha mahitaji ya maji ya dharura ambayo ni ishara ya afya mbaya [...]

07/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Somalia yahitaji kuungwa mkono ili iweze kusonga mbele: Eliasson

Kusikiliza / Somalia yahitaji kuungwa mkono, UM

Mkutano kuhusu mustakhbali wa Somalia umeanza hii leo mjini London, Uingereza ambapo Umoja wa Mataifa umeuona ni fursa ya kipekee ya jumuiya ya kimataifa kuonyesha mshikamano na Somalia na wananchi wake katika kujenga amani ya kudumu. Mkutano huo pamoja na mambo mengine unaangalia changamoto za usalama, uwajibikaji wa matumizi ya fedha na haki za kiraia. [...]

07/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jopo la UM la kuchunguza haki za binadamu DPRK latajwa

Kusikiliza / dprk-flag

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeteua tume ya watu watatu ambayo itachunguza uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Korea Kaskazini. Tume hiyo inataongozwa na mwenyekiti Michael Donald ambaye ni jaji wa zamani wa mahaka kuu nchini Australia akishirikiana na Bi Sonja Biserko wakili wa masuala ya haki za binadamu kutoka Serbia na [...]

07/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia wengi wa Syria wanaendelea kuhama makwao: OCHA

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Syria

Watu zaidi wanaendelaea kuhama ndani mwa Syria ambapo kwa kipindi cha miezi kadha iliyopita idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Syria imeongezeka mara dufu kutoka watu milioni 2 hadi watu milioni 4.25. Idadi kubwa ya wakimbizi hao wamekusanyika kweneye mji wa Aleppo na vitongozi vya mji wa Damascus kwa mujibu wa Shirika la kuratibu masuala ya [...]

07/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Visa vipya vya maambukizi ya virusi vya corona vyanainika Saudia:WHO

Kusikiliza / corona virus

Wizara ya afya ya Saudia imeliarifu shirika la afya duniani WHO kwamba kumekuwa na visa vipya vilivyothibitishwa maabara vya maambukizi ya virusi vya Novel Corona. Pia serikali hiyo imesema wagonjwa wawili walioathirika na virusi hivyo wamefariki dunia Ijumaa iliyopita huku mmoja akisalia katika hali mahtuti hospital. Kwa mujibu wa WHO uchunguzi unaendelea ambao unahusisha mlipuko [...]

07/05/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031