WFP yajitahidi kufikisha msaada wa chakula kaskazini mwa Mali hali inavyozidi kuzorota

Kusikiliza /

Hali ikizorota, WFP badi inafikisha msaada Mali

Shirika la mpango wa chakula, WFP, linafanya harakati za dharura likishirikiana na wadau wengine ili kuzifikia familia za watu ambao hawana chakula kwa sababu ya mzozo unaoendelea, hali ambayo intarajiwa kuzorota hata zaidi katika msimu unaoanza mwezi Aprili hadi Juni.Kufuatia ziara yake mjini Timbuktu wiki ilopita, Mkurugenzi wa WFP nchini Mali, Sally Haydock amesema hali ya kibinadamu ni tete, na kwamba ni vigumu kuyafikia maeneo karibu na mji wa Timbuktu kwa sababu za utovu wa usalama.

Amesema shughuli za masoko zimeathiriwa, ya chakula imepanda, kama ilivyopanda bei ya mafuta, na pesa hazipo, na hivyo watu hawawezi kununua hata bidhaa za kimsingi wanazohitaji.

WFP inaongeza usafirishaji wa chakula kwa barabara na boti za mitoni, pamoja na kuagiza chakula kutoka Niger.

WFP pia imeanzisha mpango wa kutoa chakula kwa watoto wa shule katika shule 76 kwenye eneo la Timbuktu mwezi huu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930