Watoto waendelea kutumiwa na vikundi vya wapiganaji CAR: UNICEF

Kusikiliza /

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuna taarifa kuwa watoto bado wanatumikishwa kwenye vikundi vya kijeshi, kitendo ambacho ni kinyume na haki za binadamukamaanavyoripoti Assumpta Massoi.

 (SAUTI YA MASSOI)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limesema lina ushahidi wa kutosha kuwa watoto kuendelea kutumiwa na vikundi vyenye silaha huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na imeonya viongozi wa vikundi hivyo kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.Imeelezwa kuwa zaidi ya wavulana na wasichana Elfu Mbili walikadiriwa kuhusishwa na vikundi hivyo hata kabla ya kuzuka kwa mapigano ya sasa mwezi Disemba.

UNICEF inasema kitendo cha waasi kuchukua mji mkuu Bangui hakikuzuia ukiukwaji huo wa haki za binadamu unaofanywa na pande zote zinazopigana tangu Disemba. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930