Wakimbizi Ethiopia wanajichagulia makazi na kutoa fursa za ajira

Kusikiliza /

 

Wakimbizi Dollo ado

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema maisha kwenye mahema katika kambi ya wakimbizi ya Dollo ado Ethiopia yalikuwa magumu na hatihati kwa muda mrefu.

Lakini sasa yamebadilikabaada ya wakimbizi kupata makazi mapya miongoni mwao ni bi Mako na wanawe sita.UNHCR na washirika wake wamejenga makazi 7200 ya muda katika kambi za Dollo Ado na kuwasaidia maelfu ya wakimbi. Jason Nyakundi anaripoti

 (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Makao hayo mapya ni ishara ya mabadiliko ya  huduma za dharura. Tangu mwaka 2011 sisitizo lililokuwa ni kufunguliwa kwa haraka kambi mpya na kuwapa makao wasomali 100,000 waliokimbia ukame pamoja na ukosefu wa usalama kwao nyumbani. Kambi anamoishi Kobe ilichipuka pamoja na kambi zingine mbili za Hilaweyn na Buramino. Kulishuhudiwa mabadiliko makubwa ya kambi kutoka kwa mahema ambapo picha nzima ya kambi zilibadilishwa na kutajwa kuonekana kuwa vijiji.

Hii ni baada ya Shirika la kuhudmia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kulipa kipaumbele suala la kuwahakikishia makao mazuri wakimbizi .

Mashirika matatu yanayoshirikiana na UNHCR yakiwemo baraza la wakimbzi nchini Norway na la nchini Denmark yote yalijenga makao kwa kuzingatia masuala ya kijamii na kitamaduni ya wakimbizi na hali ya hewa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29