Wahamiaji wanaorejea na wakimbizi wa Chad wahaha msimu wa mvua: IOM

Kusikiliza /

Msimu wa mvua ukitarajiwa, hali ya wakimbizi yahofiwa, Chad

Wakati msimu wa mvua unapotarajia kuanza mwezi ujao nchini Chad, hali ya maelfu ya wakimbizi na wahamiaji waliokwama katika vituo vinne vya mpaka wa Chad inaongeza kutia wasiwasi.

Yapata wahamiaji 25,000 wa Chad wamekwama kwenye kituo cha Tissi, mashariki kwenye mpaka na Sudan, baada ya kukimbia mapigano ya kikabila kati ya jamii za kiarabu za Misseria na Salamat, karibu na eneo la uchimbaji migodi la Djabal-Amir, katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Mapigano hayo yaliyoanza mnamo mwezi Janauri, yameenea hadi kwenye maeneo ya vijijini, huku magenge ya wahalifu, wakiwemo wanamgambo wa Janjaweed, yakidakia hali hiyo na kuanza kuvamia na kupora mali za wachimba migodi, wengi wao ambao ni raia wa Chad. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29