Vongozi kujadili tatizo la elimu duniani

Kusikiliza /

 

Shule DRC

Ikiwa zimebaki siku zisizozidi 1000 kufikia tarehe ilowekwa kutimiza Malengo ya Maendeleo ya Milenia mwaka 2015, viongozi mbalimbali wakiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, Rais wa Bank ya Dunia Jim Yong Kim pamoja na Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya elimu kimataifa Godon Brown, wataongoza mjadala kuhusu nini serikali na washirika wa kimataifa wafanye ili kuwapeleka watoto shule na kuboresha matokeo ya kujifunza.

Mjadala huo utawahusisha viongozi wote wa maendeleo duniani na mawaziri nane wanaowakilisha nusu ya dunia ya watoto ambao hawako mashuleni .

Nchi hizo ambazo wengi wa watoto hawajajiunga shule ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Ethiopia, Nigeria, Sudani ya Kusini, India, Yemen na Bangladesh. Mjadala huo utafanyika makao makuu ya benki ya dunia mjini Washington, Marekani Alhamisi wiki hii.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29