Vizuizi vipya Ukanda wa Gaza vyatia wasiwasi: UM

Kusikiliza /

Ukanda wa Gaza

Kufuatia kuzorota kwa hali ya usalama huko Ukanda wa Gaza katika wiki za karibuni, Israeli ilitangaza kuimarisha vizuizi vya watu na mizigo katika eneo hilo ikiwemo kufunga kivuko cha Kerem Shalom.

Hatua hiyo ya Israel imeibua wasiwasi ndani ya Umoja wa Mataifa ambapo mratibu wake wa masuala ya kibindamu James Rawley, amesema jambo hilo litasababisha kudidimia kwa akiba ya mahitaji muhimu ikiwemo vyakula, gesi na vile vile kukandamiza maisha na haki ya familia zilizoko hatarini huko Gaza.

Vizuizi vipya viliwekwa na Israeli tangu Februari mwaka huu lakini kuanzia Machi vizuizi hivyo vimejumuisha pia kupunguzwa kwa eneo la uvuvi wakati takriban familia 3500 Gaza zinategemea uvuvi kupata kipato.

Bwana Rawley amesema wanatarjia Israeli itazingatia sheria ya kimataifa, na kujizuia na masuala ambayo yanaweza kuathiri raia katika ukanda wa Gaza.

Amesema Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na Misri katika jitihada za kurejesha amani na kuangazia hali endelevu huko Gaza.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031