Utafiti wabaini tishio la uhalifu wa kimataifa Afrika Mashariki na Pasifiki

Kusikiliza /

Nembo ya UNODC

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia madawa ya kulevya na uhalifu UNODC leo inazindua tathmini ya tishio la uhalifu wa kimataifa wa kupangwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Pasifiki.

Ripoti hiyo inaangalia jinsi uhalifu huo umesababisha masoko haramu kukua sambamba na yale halali, na yanakadiriwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 90.

Masoko hayo haramu kumi na mbili yaliyoainishwa katika ripoti hiyo, yamewekwa katika makundi manne ambayo ni biashara haramu ya usafirishaji watu na uhamiajai haramu, madawa ya kulevya, wanyama pori, bidhaa za mbao na uharibifu wa tabaka la ozone pamoja na bidhaa feki na ulaghai kwenye madawa ya binadamu.

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa theluthi ya uhalifu huo wa kimataifa katika ukanda huo hufanywa katika biashara ya madawa ya kulevya ambapo mwaka 2011 tani 65 za madawa hayo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 16 zilisafirishwa, theluthi mbili kati ya hizo zikiwa zimetengenezwa nchini. Myanmar.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29