Mtaalamu maalum wa UM kuhusu ukatili dhidi ya wanawake atazuru India

Kusikiliza /

Rashida Manjoo

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Rashida Manjoo atakuwa na ziara ya zaidi ya wiki moja nchini India kuanzia wiki ijayo, kubwa zaidi ni kutathmini vitendo dhalili dhidi ya wanawake nchini humokamaanavyoripoti George Njogopa.(TAARIFA YA GEORGE)

Kwa mujibu wa Bi Manjoo unyanyasaji wa kijinsia unaendelea kusalia ,moja ya tatizo kubwa linalokwaza haki za binadamu likiathiri kila nchi duniani kote.

Akielezea India, Mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa taifa hilo liko kwenye mkondo mzuri wa kihistoria kuyatafutia ufumbuzi masuala yanayohusu unyanyasaji dhidi ya wanawake na wakati huo huo kusaka shabaha kutoa usawa kwa makundi ya wanawake.

Akiwa nchini  India, Bi Manjoo anatazamia kukutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali pamoja na wawakilishi wa vyama vya kiraia, wakati atapotembelea miji ya Delhi, Rajasthan,Gujarat, Tamil Nadu. 

Aidha ameeleza kuwa ziara yake hiyo ya siku kumi,itafungua njia ya kuwa na majadiliano ya mezani baina ya viongozi wa kiserikali na wale kutoka taasisi binafsi.

Mwishoni mwa ziara yake anatazamia kukutana na waandishi wa habari ambako atajadilia yale yatakaojiri wakati wa ziara hiyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031