Umoja wa Mataifa wasitisha ugawaji wa chakula Gaza:

Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa umesitisha kwa muda mipango yote ya ugawaji wa chakula Gaza baada ya waandamanaji kuvamia moja ya vituo vya kama inavyoarifu taarifa iliyoandaliwa na Flora Nducha.

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

Shirika la Umoja wa mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema uvamizi uliofanyika kwenye moja ya vituo vya Gaza ambao unaonekana ulipangwa ni kitendo kisichokubalika.

UNRWA inasema misaada yote na vituo vya ugawaji vitasalia kufungwa hadi pale watakapohakikishiwa na pande zote kuwa operesheni zao zitaweza kuendelea bila bughdha.

Wapalestina wapatao 800,000 wanafaidika na ugawaji wa chakula Gaza lakini UNRWA hivi sasa inakabiliwa na upungufuwa dola milioni 67.2 katika kufanikisha azma yake.Sami Mshasha ni msemaji wa UNRWA

(CLIP YA SAMI MSHASHA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930