Umoja wa Mataifa wahofia hali tete ya usalama Israel:Serry

Kusikiliza /

 

Robert Serry

Mratibu maalumu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati Robert Serry amesema anatiwa hofu na hali tete, kufuatia kuanza upya kuvurumishwa maroketi kutoka Gaza kwenda Israel jana na leo asubuhi, na pia kuendelea kwa mvutano dhidi ya suala la wafungwa ambalo halijapata suluhu.

Amesema ni muhimu kwa pande zote kujizuia na ghasia katika wakati huu na kushirikiana kushughulikia masuala yanayohitaji ufumbuzi. Ukiukwaji wa kusitisha mapigano unaweka hatarini muafaka uliofikiwa baina ya Israel na Gaza Novemba 21 na kuweka matatani mafanikio machache ya usalama yaliyoanza kufikia Gaza na Kusini mwa Isarel.

Umoja wa Mataifa unaalani vikali uvurumishaji huo wa makombora hasa katika maeneo ya raia na kutoa wito kwa Israel kutochukua hatua ya kulipiza, pia umesema utaendelea kuunga mono juhudi za Misri za kurejesha utulivu na kuhakikisha makubaliano ya kusitisha mapigano yanatekelezwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930