UM yalaani vikali mauaji ya walinda amani na wafanyakazi wake Sudan Kusini

Kusikiliza /

Majeruhi wa mashambulizi Sudan Kusini

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, amelaani vikali tukio la kuuwawa kwa askari watano waliokuwa kwenye kikosi cha ulinzi wa amani.
Hilde Johnson amesema kuwa watumishi hao waliokuwa wakifanya kazi kwenye ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusin UNMISS walivamia na watu wasiojulikana wakati wakiwa karibu na makazi yao huko Gumuruk, jimboni Jonglei.
Katika tukio hilo walinzi wengine wa amani walijeruhiwa na wengine hali zao bado ni mbaya.
Bi Johnson ameelezea masikitiko yake na ametuma salama za rambi rambi kwa ndugu na jamaa waliofikwa na msiba huo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031