UM waitaka Iraq kusitisha unyongaji watu

Kusikiliza /

 

Unyongaji watu usitishwe,UM

Jumla ya watu 33 wamenyongwa nchini Iraq mwezi uliopita huku wengine 150 wakitarajiwa kunyongwa siku zinazokuja kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.Serikali ya Iraq inashikilia msimamo wake kuwa wanaonyongwa ni wale wanaohusuka kwenye vitendo vya kigaidi na uhalifu mwingine dhidi ya raia.

Mkuu wa haki za binadamu kweneye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa hakuna uwazi kutokana na jinsi hukumu zinavytolewa.

Anasema kuwa mfumo wa sheria nchini Iraq una utata mwingi kwa rufaa. Rupert Colvile ni msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

"Kuna hukumu nyingi zinazotolewa kutokana na kukiri baada ya kuteswa na kudhulumiwa. Mahakama bado ni dhaifu na kesi mara nyingi zinakosa viwango vya kimataifa. Kamishina mkuu amesisitiza kuwepo kwa uwazi na kuheshimiwa kwa sheria. Anatoa wito kwa serikali kusitisa kunyongwa huku na kufanya uchunguzi wa kesi zinazohusu kunyongwa na kufichua habari kuhusu idadi ya wafungwa wanosubiri kunyongwa, mashataka na kesi dhidi yao na matokeo ya uchunguzi wa kesi zao."

Ofisi ya Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa kuna zaidi nya watu 1400 wanaosubiri kunyongwa nchini Iraq.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2016
T N T K J M P
« jul    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031