Uchumi wa nchi zenye kipato cha chini umeimarika mara dufu-IMF

Kusikiliza /

Uchambuzi uliofanywa na jopo la wataalamu wa fuko la fedha duniani IMF unaonyesha kuwa nchi ambazo zinatajwa kuwa katika kiwango cha kipato cha chini, zimeimarika na kufanya vizuri katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Wachambuzi hao ambao wametoa hali ya mwelekeo ya uchumi wa dunia, wamesema mataifa hayo yenye kipato cha hali ya chini yamefanakiwa kuboresha uchumi wao na sasa umeimarika zaidi ukilinganisha na vile ilivyokuwa katika miaka 1990.

Mataifa hayo yamefaulu kusimamia vyema mapato na matumizi ya sekta za umma huku pia yakianzisha mageuzi kwa shabaha ya kuupa msukumo mpya uchumi wa taifa

Wachambuzi hao wamezita nchi kama Indonesia na Korea kama ni za mfano kwai baada ya kuandamwa na hali mbaya ya kiuchumi katika miaka ya 60 zilikaribisha mageuzi ambayo baadaye yalizaa matunda.

Hali hiyo ndiyo iliyoshuhudiwa sasa kwa mataifa hayo yenye kipato cha chini ambayo yamekaribisha mageuzi na kuzingatia mifumo ya matumizi jambo lililosaidia kuimarisha uchumi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29