Twahitaji dola Milioni 19 kila wiki kuhudumia wakimbizi wa Syria: WFP

Kusikiliza /

Wakati wa vitafunio, Syria

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limesema linaweza kulazimika kupunguza msaada wake kwa wakimbizi wa Syria iwapo halitapatiwa fedha zaidi.WFP imesema itahitaji dola Milioni 18 kwa miezi mitatu ijayo ili operesheni zake za usaidizi wa chakula hukoSyria na nchi jirani zinazohifadhi wakimbizi ziweze kuendelea hata baada ya mwezi Juni.

Shirika hilo limesema mathalani mpango wa kuwapatia vocha za chakula wakimbizi walioko Jordan na Lebanon unaweza kusitishwa mwezi ujao kutokana na  ukata.

Elizabeth Byrs ambaye ni msemaji wa WFP amesema ukosefu wa utashi wa kisiasa kwenye mzozo wa Syria na kupungua kwa msaada wa kifedha kwenye mpango wa dharura unakwamisha uwezo wa mashirika ya misaada kukidhi  mahitaji.

(SAUTI YA BYRS)

 "Kushindwa kukidhi mahitaji ndani ya Syria itakuwa ni kichocheo cha kuwa na wakimbizi zaidi na itakuwa gharama zaidi kukidhi mahitaji yao kwa siku za usoni. Pesa za vocha za vyakula nchini Jordan zinatosheleza hadi katikati ya mwezi Mei. Baada ya hapo kama hatupati fedha tutalazimika kupunguza thamani ya vocha na hiyo itatosheleza kwa wiki mbili tu badala ya mwezi mzima husika na hivyo kuathiri wakimbizi wapatao 175,000 wa Syria wanaoishi na wenyeji huko Jordan."

WFP inatoa msaada kwa zaidi ya watu Milioni Mbili na Nusu ndani na nje ya Syria na zaidi ya wakimbizi Milioni moja waSyria wakoJordan,Lebanon, Uturuki na Iraq.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930