Tukishindwa kulinda mazingira, tumeshindwa kulinda haki za binadamu," waonya wataalamu wa UM

Kusikiliza /

Ni lazima tulinde mazingira yetu, wataalamu, UM

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wameonya kuwa, iwapo dunia itashindwa kulinda mazingira, basi itakuwa imeshindwa pia kulinda na kuzitetea haki za binadamu.

Wakizungumza mjini Geneva kwenye kilele cha siku ya dunia, wataalamu hao wamesema kuwa kadri binadamu anavyoshindwa kuyatunza mazingira ndivyo anavyozalisha janga litakalomfanya ashindwe kufurahia haki za msingi za binadamu,

Ikiwa imepita miongo kadhaa tangu kuasisi kwa siku ya dunia, iliyoanza kuzingatiwa kwa mara ya kwanza April 22 mwaka 1970, wataalamu hao wamesema kuwa kuzitafutia ufumbuzi changamoto zitokanazo na uharibifu wa mazingira ni kusema kwamba binadamu inazijibu changamoto za afya, chakula, maji safi na salama.

Wamesema kuwa kwa kuchukua hatua ya kulinda mazingira dunia itakuwa imefaulu kukabiliana na changamoto zinazotia kutoweka kwa baadhi ya viumbe pamoja na makundi ya watu walioko pembezoni.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2015
T N T K J M P
« ago    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930