Tathmini ya ugonjwa wa homa ya mafua ya ndege China yakamilika

Kusikiliza /

Uchunguzi wa homa ya mafua ya ndege

Jopo la wataalamu wa kimataifa na wa China lililofanya ziara ya kutathmini hali ya ugonjwa wa mafua ya ndege aina ya H7N9 nchini humo na hatimaye kutoa mapendekezo limehitimisha kazi yake ambapo kwa kiasi kikubwa limesema hatua zilizochukuliwa kudhibiti ugonjwa huo zinatia moyo.  Ziara hiyo ilifanyika katika majimbo ya Shanghai naBeijingambapo Mkurugenzi msaidizi kutoka Shirika la Afya duniani, WHO Dkt. Keiji Fukuda amesema hatua zilizochukua naChinani mfano wa kuigwa.  Amesema taasisi zote husika za umma zilibadilishana taarifa mapema katika ngazi mbali mbali na ni dhihirisho la uthabiti wa mfumo wa upashanaji taarifa waChinana jinsi ambavyo imewekeza vyema katika mfumo wa afya. 

Hata hivyo, jopohilolimeonya kuwa wataalamu bado wana uelewa usio timilifu kuhusu kiwango cha ugonjwa huo ambao hadi sasa umesababisha vifo.

 

Jopohilolimesema hata hivyo halijapuuza uwezekano wa kirusi hicho cha H7N9 kuweza kuambukizwa kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu na wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa kitaifa na kimataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031