Taasisi za UM zaungana kuboresha hali ya udongo katika ardhi kame

Kusikiliza /

Umuhimu wa kuhifadhi udongo

Taasisi mbili za Umoja wa Mataifa zimetiliana saini mradi wa kutumia teknolojia ya nyuklia kutathmini hali ya udongo katika ardhi kame, kama njia mojawapo ya kuepusha mmomonyoko wa ardhi.Shirika la nishati ya atomiki duniani, IAEA na taasisi ya Umoja wa Mataifa ya kusimamia mkataba wa kudhibiti na kuzuia kuenea kwa jangwa duniani, (UNCCD) wametia saini mkataba huo huko Bonn Ujerumani wakati huu ambapo mmomonyoko wa ardhi unatishia uhai wa watu zaidi ya Bilioni Moja na Nusu duniani kote.

Afisa kutoka IAEA Claudia Raffo-Caiado amesema shirika hilo linatoa stadi za kutafiti matatizo ya mmomonyoko wa ardhi na udongo na suala hilo ni muhimu katika kuhifadhi udongo, kupanga na kufanya uamuzi kuhusu matumizi ya ardhi.

Mradi huo utakaotekelezwa hadi mwezi Disemba mwaka 2017 unalenga kuimarisha uhifadhi wa ardhi na rasilimali za udongo na hivyo kuunga mkono jitihada za kutokomeza umaskini, uhifadhi endelevu wa mazingira na kuboresha hali ya udongo katika maeneo kame.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031