Taa za kutumia nishati ya jua kukabiliana na ubakaji Somalia

Kusikiliza /

 

Wakimbizi katika moja ya kambi mjini Mogadishu

Katika kupambana na ukatili wa kijinsia nchini Somalia, Shirika la kimataifa la masuala ya umeme la nchini Japan, Panasonic, kwa kushirikiana na shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM,  limeanzisha utafiti wa namna taa za kutumia nishati ya miale ya jua zinavyoweza kupunguza ukatili huo katika kambi za wakimbizi na wahamiaji . Mchango huo wa kiasi cha dola za Marekani elfu 31 unafuatia uchunguzi usio rasmi  wa IOM wa mwaka 2012 ulioonyesha  kuwa asilimia kubwa ya vitendo vya ukatili ikiwamo ubakaji hufanyika usiku katika makambi wakati kukiwa na giza .  Joseph Msami amefanya mahojiano na msemaji wa shirikia la kimataifa la uhamiaji  IOM Jumbe Omari Jumbe ambaye anaanza kwa kueleza nini hasa shirika hilo litafanya katika utafiti huo wa kisayansi unaolenga kupambana na ukatili wa kijinsia katika nchi ambayo kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji, ubakaji unaripotiwa kwa kiwango cha juu kuliko nchi nyingine duniani. (MAHOJIANO)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031