Suluhu la kisiasa Darfur bado kupatikana: Ladsous

Kusikiliza /

Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limeleezwa kuwa miaka Kumi tangu mzozo wa Darfur utambulike kimataifa bado suluhu ya kisiasa haijapatikana na hali ya usalama kwa watendaji wa Umoja wa Mataifa inatia wasiwasi. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa Herve Ladsous akisoma ripoti ya Katibu mkuu kuhusu hali ya utendaji kazi ya ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID kwa miezi mitatu iliyopita, amesema majukumu ya chombo hicho yanakwamishwa na kuzorota kwa usalama.

Amesema hata utekelezaji wa makubaliano ya Doha kati ya serikali ya Sudan na kundi la Liberation and Justice Movement bado haujawa dhahiri kwa lengo la kuleta amani na kuwezesha usambazaji wa misaada ya kibinadamu.

(SAUTI YA LADSOUS)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031