Suala la kurejeshwa makwao kwa Wakimbizi wa Rwanda laangaziwa

Kusikiliza /

Wakimbizi wa Rwanda kurudi nyumbani kwa hiari

Mkutano wa mawaziri wa Afrika uliofanyika Pretoria wazungumzia hatma ya wakimbizi wa Rwanda kurejea makwao kwa hiari kama anavyoripoti Joseph Msami

(TAARIFA YA MSAMI)

Nchi kadhaa za Afrika zinazohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi wa Rwanda pamoja na Rwanda, zimeelezea dhamira zao za kutatua tatizo la muda mrefu la wakimbizi wa Rwanda, kwa mujibu wa mkakati wa kina ambao ulitangazwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR, Mwezi Oktoba mwaka 2009.

Katika mkutano wa Mawaziri huko Pretoria Afika Kusini, wajumbe kutoka Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Afrika Kusini, Uganda, Zambia, na Zimbabwe wamepitia upya maendeleo ya kuwarudisha makwao wakimbizi kutoka Rwanda na kuwaunganisha tena na jamii zao.

Mkakati wa UNHCR unatoa ukomo wa hadhi ya wakimbizi wa Rwanda waliosalia uhamishoni na ambao walikimbia nchi yao kabla ya tarehe 31 Desemba mwaka 1998

Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN)

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031