Siku ya afya duniani; Shinikizo la damu ni tatizo kubwa: WHO

Kusikiliza /

Siku ya afya duniani 2013

Siku ya afya duniani, tarehe Saba mwezi Aprili mwaka huu wa 2013 imetajwa mahususi kumulika shinikizo la damu.  Shinikizo la damu limetajwa kuwa chanzo cha magonjwa mengi yanayohusiana na kushindwa moyo kufanya kazi yake. Shirika la afya duniani, WHO linaeleza kuwa mtu mmoja kati ya watu wazima watatu ana shinikizo la damu na wengi wao hawajitambui kwa kuwa ni mara chache dalili kujitokeza. Na zaidi ya yote nusu ya vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo au kiharusi hutokana na shinikizo la damu na mwelekeo ni kwamba hali itazidi kuwa mbaya iwapo hatua hazitachukuliwa. Je ni hatua zipi hizo? Basi ungana na Assumpta Massoi katika makala haya.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2016
T N T K J M P
« jun    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031