Sheria ya Hungary kudhibiti wasio na makazi yapingwa

Kusikiliza /

 

Magdalena Sepulveda

Wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya umaskini na makazi wameshutumu mabadiliko ya sheria nchini Hungary inayopiga marufuku mtu kulala kwenye sehemu za umma.

Wataalamu hao wa haki za binadamu wametaka serikali ya Hungary kutupilia mbali sheria hiyo kumbatana na uamuzi ulitolewa wa mahakama wa kutaka kutotambuliwa kama kosa hali ya kutokuwa na makao.

Wataalamu hao wameelezea wasi wasi wao kutokana na sheria hiyo iliyopitishwa bila ya kutoa fursa kwa umma kutoa maoni yao. Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu umaskini na haki za binadamu Magdalena Sepúlveda anasema kuwa sheria kama hiyo itakuwa yenye athari kwa watu maskini na wale wasio na makao.

Kwa upande wake mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu makao Raquel Rolnik amesema kuwa kulingana na serikali ya Hungary ni kwamba kwa sasa hakuna makao ya kutosha kwenye mji mkuu ya kuwatosha wasio na makao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031