Pima shinikizo la damu yako, punguza hatari: WHO

Kusikiliza /

upimaji wa shinikizo la damu

Takriban watu bilioni moja kote duniani wanakadiriwa kuathiriwa na shinikizo la damu, hali ambayo inaathiri kila mtu mmoja kati ya watatu wenye umri wa zaidi ya miaka 25.

Idadi kubwa zaidi ya watu walioathirika na shinikizo la damu wapo barani Afrika, linakoathiri asilimia 46 ya watu wazima.

Kwa mujibu wa WHO, shinikizo la damu ni moja ya vitu vinavyochangia zaidi ugonjwa wa moyo na kiharusi, ambavyo kwa pamoja huchangia kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo vya mapema na ulemavu. Shinikizo la damu pia huongeza hatari ya kuharibika figo na upofu.

Kabla ya Siku ya Afya Duniani, Aprili Saba, WHO imewataka watu wapime  na kuzuia au kudhibiti shinikizo la damu. Daktari Shanthi Mendis ni mtaalamu wa WHO.

(SAUTI Dr. Mendis )

"Mara nyingi hakuna dalili, hadi unapopata matatizo. Watu wanatakiwa wajue vipimo vyao. Kupunguza ulaji wa chumvi katika vyakula, kula matunda na mboga, kupunguza matumizi hatari ya pombe, kufanya mazoezi ya kudhibiti uzito na kuhakikisha huli chakula kingi na kuongeza uzito- vyote hivi vinachangia kuzuia shinikizo la damu"

 

 

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031