Pamoja na kupiga hatua kwenye malengo ya milenia, lakini tatizo la njaa bado ni kubwa-FAO

Kusikiliza /

José Graziano da Silva

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la chakula ulimwenguni FAO José Graziano da Silva amesema serikali pamoja na viongozi wa kitaifa wanaowajibu mkubwa wa kuwahakikishia wananchi wao usalama wa chakula.

Akizungumza kwenye mkutano unaowakutanisha maafisa wa ngazi za juu wanaomulika mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuelekea mwaka 2015, da Silva amesema kimsingi kuwepo kwa malengo ya maendeleo ya mellenia kumesaidia kwa kiwango kikubwa kuzisukuma nchi  nyingi kusonga mbele, lakini pamoja na hali hiyo bado kuna mamilioni ya watu wanakabiliwa na tatizo la njaa.

 

Alisema kiasi cha watu milioni 870 duniani wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula hivyo akasema kuwa vita vya kukabiliana na tatizo la njaa bado inasafari ndefu.

 

Alisema jawabu sahihi la kukabiliana na hali hiyo ni kuwepo kwa utashi wa kisiasa katika ngazi zote, kitaifa mpaka kwenye duru la kimataifa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930