Mzozo Jamhuri ya Afrika ya Kati wasababisha maelfu ya wakimbizi

Kusikiliza /

Mashirika ya kutoa misaada yanaripoti kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wanaokimbilia nchi jirani.

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema idadi ya wakimbizi hao imepanda na kuzidi 37, 000 katika wiki chache zilizopita, wengi wao wakikimbilia Chad, Cameroon, na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).

UNHCR inasema kuongezeka kwa mapigano mnamo mwezi Disemba mwaka ulopita na kupinduliwa kwa serikali na waasi mwezi Machi kumewalazimu takriban watu 175, 000 kuhama makwao ndani ya nchi.

Shirika hilo pia linasema mahitaji ya kibinadamu ni mengi, kwani wengi wao walikimbia bila chochote, na wanaishi na familia ambazo tayari zinahangaika na umaskini ulokithiri. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

UNHCR imesema haijaweza kutoa misaada ya kibinadamu inayotosha kwa wakimbizi wa ndani CAR kwa sababu za kiusalama.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930