Mwakilishi wa UM kuhusu ukatili wa kimapenzi kwenye migogoro azuru Mogadishu:

Kusikiliza /

Hawa Bangura

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi kwenye maeneo ya vita Zainab Hawa Bangura amewasili Moghadishu ili kuhamasisha na kujadili njia za kukabiliana na tatizo la ukatili wa kimapenzi Somalia , kama anavyoarifu Alice Kariuki.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Bi Bangura amekutana na maafisa wa Umoja wa mataifa , jumuiya za kijamii na na wadau wengine ili kusikiliza na kujifunza kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo katika kushughulikia tatizo la ukatili wa kimapenzi. Ziara yake hii ambayo ni ya kwanza nchini Somalia ina lengo la kukusanya taarifa zitakazosaidia majadiliano na serikali. Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano pia amewapongeza waandishi habari wa Somalia kwa kutanabaisha tatizo hilo na kuwaambia kwamba wanajukumu kubwa la kuelimisha. Ameongeza kuwa jopo la wataalamu kutoka ofisi yake wataenda Somalia Julai mwaka huu kushirikiana na kamisna wa polisi na jeshi kufanya tathimini kwa ajili ya kutoa msaada, mafunzo na pia kuwachukulia hatua wahusika.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031