Mustakhbali wa nyuklia wajadiliwa na mawaziri Petersburg:IAEA

Kusikiliza /

Mawaziri kukutana kujadili mustakhbali wa nyuklia

Mawaziri wa serikali mbalimbali na wataalamu wa kimataifa wanakutana mjini Persburg Urusi kuanzia June 27 hadi 29 mwaka huu kujadili mustakhbali wa nyuklia. Maelezo zaidi na George Njogopa (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kongamano hilo linashabaha ya kutoa fursa kwa watunga sera pamoja na wataalamu wengine kujadilia kwa kina nafasi na uwezekano wa matumizi ya nguvu za kinuklia kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Mada inayozingatiwa ni katika maeneo ya upunguzaji wa janga lilohisiana na mabadiliko ya tabia nchi, na kuweka viwango vinavyokubalika kimataifa juu ya matumizi ya nishati za kinuklia kwa ajili ya uzalishaji umeme.

Lakini pia wataalamu hao wataangazia nafasi ya matumuzi ya mitambo ya kinuklia namna inavyoweza kuwa salama zaidi na kukifaa kizazi cha usoni na kuanzisha mipango ya kiufundi.

Mkutano huo ambao umeandaliwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya shirika la Umoja wa Mataifa la nguvu za atomiki,wakala wa kimataifa wa nguvu za nuklia, na serikali yaRussiaunatazamiwa kuwa mijadala ya ndani ambako taarifa mbalimbali zinatazamiwa kutolewa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Febuari 2016
T N T K J M P
« jan    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
29