Malala Yousfzai azungumza na Ban, amwelezea afya yake

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon katika mazungumzo na Malala Yousfzai kwa njia ya mtandao

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo kwa njia ya mtandao na mtoto Malala Yousfzai ambaye alijeruhiwa kwa risasi na watalibani huko Pakistani mwezi Oktoba mwaka jana kutokana na msimamo wake wa kutetea bayana elimu kwa mtoto wa kike. Katika mazungumzo hayo Bwana Ban ameelezea kufurahishwa kwake kwa kumuona Malala akiwa mwenye afya njema huku Malala akitoa shukrani kwa watu wote duniani akiwemo Katibu Mkuu kwa kumuombea afya njema.

(SAUTI MALALA)

"Ndio niko na afya njema na ni kwa sababu watu wote duniani,  hususan wewe mlikuwa mkiniombea maisha mema. Hii leo naweza kuchezesha mikono yangu, naweza kuongea, naweza kutembea naweza kufanya kitu chochote kile hata kwenda shule.".

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031