Mkuu mpya wa UNAMID aanza kazi Sudan:

Kusikiliza /

Mohamed Ibn Chambas

Mkuu mpya wa mpango wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika kulinda amani Dafur UNAMID Mohamed Ibin Chambas amewasili Khartoum kuanza majukumu yake.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Mkuu mpya wa kikosi cha pamoja cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za Afrika UNAMID Mohamed Ibn Chambas amewasili mjini Khartoum kuanza rasmi majukumu yake kama kamanda wa kikosi cha UNAMID kwenye jimbo la Darfur.

Akizungumza baada ya kuwasili, Chambas amesema kuwa ana furaha ya kuchukua wadhifa huo  kwenye jimbo la Darfur wakati huu akiongeza kuwa  amani  kuambatana na makubaliano ya Doha inaweza kuleta suluhu la kudumu  kwa mamilioni ya watu wanaotaabika katika eneohilo.

Chambas anachukua wadhifa huo kutoka kwa Ibrahimu Gambari na kati ya majukumu yake ni kuwa mpatanishi mkuu wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za Afrika.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031