Mkutano wajadili nafasi ya wanawake katika kudhibiti migogoro Sahel

Kusikiliza /

Wakazi wa Ukanda wa Sahel barani Afrika

Mkutano ni hatua ya kwanza ya kuhakikisha kuwa sauti za wanawake kutoka eneo la Sahel zinasikika na kuwa maoni yao yanatiliwa maanani. Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Sahel Romano Prodi anasema kuwa wanawake katika eneo la Sahel  watakuwa kiungo muhimu katika utulivu wa eneohilo. Mjumbe kutoka kwa Jumuiya ya Ulaya  Catherine Ashton anasema kuwa  wakati mwanamke anapopiga hatua jamii nazo hupiga hatua , penye wanawake huteseka jamii huteseka pia. Mapendekezo ya mkutano huo yatawasilishwa kwemye mkutano wa wafadhili utakaondaliwa mjiniBrussels. Kati ya mapendekezo yaliyowekwa kuhakikisha kuwepo amani , usalama na maendelo eneo laSahelwashiriki walisisitiza  umuhimu wa kuhakikisha kuwa asilimia 30 ya washiriki wa kutoa maamuzi ni wanawake.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031