Mjumbe maalumu wa UM ahitimisha ziara yake ya kwanza Somalia

Kusikiliza /

Bi. Zainab Hawa Bangura

Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika unyanyasaji wa kingono kwenye maeneo yaliyokumbwa na machafuko Zainab Hawa Bangura  amekamilisha ziara yake ya kwanza nchini Somalia ambako amekutana na kufanya mazungumzo na makundi mbalimbali ya watu.

Katika ziara yake hiyo Bi Bangura pia amekutana na mawaziri, Maafisa wa AMISOM, majaji na maafisa wa kijeshi.

Shabaha kubwa ya ziara hiyo na kujionea hali jumla ya mambo pamoja na kupata taarifa sahihi kuhusiana na watu waliokumbwa na madhira wakati wa vita kabla ya kuanza majadiliao na maafisa wa serikali katika siku za usoni.

Akizungumzia ziara yake hiyo, Bi Bangura amesema kuwa ilikuwa fursa muhimu kutembelea taifa hilo ambalo sasa linaanzisha enzi mpya baada ya kuandamwa na vita kwa miaka mingi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2017
T N T K J M P
« dis    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031