Miaka 27 baada ya zahma ya Chernobly athari bado zipo:Ban

Kusikiliza /

 

KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anasema wakati leo dunia ikikumbuka zahma ya Chernobly miaka 27 iliyopita ni muhimu kuwaenzi wafanyakazi wa huduma za dharura waliosaidia wakati wa ajali hiyo ya nyuklia mbaya kabisa kuwahi kutokea na kukatli maisha ya watu wengi huku zaidi ya 330,000 kulazimika kuzihama nyumba zao. Anasema mamilioni ya watu walioathirika na mionzi daima hawatosahaulika. Maeneo yaliyokumwa na zahma hiyo hadi leo yanashuhudia athari, ikiwemo za kimazingira hasa katika vyakula, ardhi na maji ambazo zitaendel;ea kwa muda. Lakini amesema jamii za eneo hilo hivi sasa zina fursa ya kuweza kuishi maisha ya kawaida waathirika wanaonyesha matumaini makubwa ya siku za usoni japo wataendelea kuhitaji msaada wa kimataifa.

Kutokana na zahma hiyo Ban anasema jumuiya ya kimataifa imejifunza mengi zikiwemo athari za nyuklia kwa maisha ya binadamu na jinsi ya kukabiliana na tisho la nyuklia. Ban anasema ingawa miaka 27 imepita tangu ajali ya Chernobly Umoja wa mataifa utaendelea kuwasaidia waathirika na kushirikiana na nchi wanachama kuhakikisha usalama wa nyuklia na maendeleo endelevu ya nishati kwa wote.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031