Mgogoro wa uchumi wachochea ukosefu wa ajira Ulaya:ILO

Kusikiliza /

 

ukosefu wa ajira

Mkutano wa  tisa  wa shirika la kazi duniani ILO kanda ya Ulaya umeanza rasmi mjini Oslo huku wito ukitolewa wa kutaka kuwepo kwa sera zinazoweza kuchangia kubuniwa kwa ajira zilizo bora.

Waziri Mkuu nchini Norway  Jens Stoltenberg anasema kuwa mgogoro wa kiuchumi  barani Ulaya umesababisha kuwepo kwa ukosefu mkubwa wa ajira.

Anasema kuwa Watu zaidi wanaendelea kubaki bila ajira na kusababisha hali inayotajwa kuwa ya kupotea kwa kizazi hiki. Naye mkurugenzzi mkuu wa ILO Guy Rider ni kuwa changamoto zilizo kwa sasa ni za kichumi na  ajira pasipo na suluhu lolote , akitaka mkutano huo kutoa mapendekezo yatakayopelekea kupatikana kwa suluhu.

Kulingana na takwimu za hivi punde za ILO ni kwamba mgogoro uliopo umewaacha zaidi ya watu milioni 26.3 barani Ulaya bila ajira ikiwa ni milioni 10.2 zaidi tangu kuanza kwa mgogoro huo mwaka 2008.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930